MUZIKI KAMA SANAA
Muziki ni sanaa kama zilivyo sanaa nyingine. Tofauti ya muziki na Sanaa nyingine ni matumizi ya ala ambayo imekuwa na mvuto kwa watu wengi, hii pia imewafanya wengi kuvutiwa na aina hii ya sanaa. Sanaa hii kama zilivyo sanaa nyingine inahitajika kufanywa kwa ubunifu na weledi wa hali ya juu kiasi kwamba haiwezi kupoteza ubora wake ndani ya muda mfupi (kuchuja). Rai yangu kwa wanamuziki, tutunge nyimbo ambazo kizazi cha kesho na keshokutwa kitaona fahari kwa kazi hizo. Nawatakia utunzi mwema.